Hapo zamani za kalekuliishi ndovu mwenye majivuno sana. Alitembea kwen ye mwitu aking’oa miti zote zile alizipata mbele yake. Wakati aliguruma, wanyama wote walitetemeka.
- Mimi ndiye mnyama mkubwa zaidi katika mwitu – aliguruma. Mimi ndiye mwenye nguvu zaidi. Ninyi wanyama wote lazima mniheshimu na mniogope.
Siku moja alipokuwa akitembea na kugonga miguu yake kila mahali, alizisikia sauti ndogo zikiita:
-
Tafadhali tazama unakoweka miguu la sivyo utatuua.
- Haa! Haa! Haa! Alicheka. Ninyi ni wadogo sana na ziwezi kuwaona. Hamna aibu ya udogo wenu? Haa! Haa! Haa!
- Tunapenda kujivunia udogo wetu – walijibu siafu -, sisi kufanya kazi zaidi ku
washinda ninyi wanyama wakubwa na wavivu.
- Nikiuzungusha mara moja huu mkonga wangu, naweza kufanya kazi zaidi ya ile ninyi mwaweza kuota kufanya maishani mwenu – ndofu alijivuna – Haa!Haa!Haa! Ninyi ni siafu bila faida.
Kucheka kwake kulisikika kwenye msitu wote na kuwanyamazisha nyani wote waliokuwa wakilia. Mda mfupi baadaye, ndovu alijipata kwenye mtego. Alijaribu kujiweka huru lakini hakufaulu. Alizidi kujizungusha kwenye mtego huo. Miguu yake ilibaki hewani na masikio yake makubwa yalifagia sakafu. Akaanza kulia akitafuta usaidizi.
Simba alipita na akamsikia ndovu akilia.
-
Tafadhali nisaidie! Niweke huru! - alilia.
Simba alimwangalia na akakitingisha kichwa chake.
-
Sidhani kama naweza kukusaidia rafiki yangu. Lazima nitoroke kabla wanadamu waje waniuwe pia.
Simba akatoroka na kumwacha.
Baada ya mda mfupi akapita nyati na akamisikia ndovu akilia.
-
Tafadhali nisaidie nyati la sivyo nitauawa – ndovu alimlilia nyati.
Nyati alimwangalia na kumjibu:
-
Lazima nitoroke kabla wanadamu waje kuniua – akaenda zake.
Ndovu alilia akiwa na hasira na uoga mingi. Akasikia sauti ndogo ikitetemeka ikisema:
-
Inaonekana una shida, naweza kukusaidia?
Ndovu aliangalia kila mahali, mwishowe akamwona siafu.
-
Oh! Ni wewe! – alilia – iwezi kutoka kwenye mtego huu. Simba, nyati, kifaru, na nguruew hawawezi kunisaidia. Wewe waweza?
-
Ndio – alijibu siafu.
-
Wewe ni mdogo sana – alisema ndovu – lakini kama waweza kunisaidia, tafadhali fanya hivyo.
-
Sawa – sauti ndogo ikasema – ningoje nardi sasa hivi.
Siafu aliondoka na baada ya mda mfupi alirudi na wenzake. Walizila kamba zote zilizomfunga ndovu na wakamweka huru.
Ndovu alikosa maneno ya kuwashukuru siafu kwa kazi ambayo walikuwa wamefanya. Alikuwa amewachekelea. Aliapa hatafanya hivyo tena na tangu siku hiyo alishika adabu.
|